1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya wataka uchaguzi wa rais wa Senegal ufanyike

4 Februari 2024

Umoja wa Ulaya umetoa wito kwa wahusika wote nchini Senegal kushirikiana pamoja kwa ajili ya kuandaa uchaguzi wa haki na uwazi, jumuishi na wa kuaminika haraka iwezekanavyo.

https://p.dw.com/p/4c1on
Rais wa Senegal Macky Sall
Rais wa Senegal Macky SallPicha: RTS/Reuters

Umoja wa Ulaya umetoa wito kwa wahusika wote nchini Senegal kushirikiana pamoja kwa ajili ya kuandaa uchaguzi wa haki na uwazi, jumuishi na wa kuaminika haraka iwezekanavyo.

Msemaji wa Umoja wa Ulaya, kwa Sera ya Mambo ya Nje na Usalama Nabila Massrali ametoa tamko hilo leo Jumapili kabla ya maandamano ya upinzani yanayotarajiwa kufanyika mjini Dakar.

Makao makuu ya Umoja wa Ulaya mjini Brussels, Ubelgiji
Makao makuu ya Umoja wa Ulaya mjini Brussels, UbelgijiPicha: James Arthur Gekiere/Belga/dpa/picture alliance

Msemaji huyo wa Umoja wa Ulaya amesema kuahirishwa kwa uchaguzi wa rais nchini Senegal kunafungua kipindi cha kutokuwa na uhakika nchini humo.

Rais Macky Sall wa Senegal alitangaza kuahirishwa kwa uchaguzi uliopangwa kufanyika Februari 25 kwa muda usiojulikana, kwa kile alichokitaja kuwa ni kuanzishwa kwa uchunguzi dhidi ya madai ya rushwa miongoni mwa wagombea.

Rais Macky Sall hakutoa tarehe maalum ya uchaguzi lakini alisema majadiliano ya kitaifa yatafanyika ili kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru, wa wazi na shirikishi.