1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSenegal

Baraza la Katiba Senegal lakataa maombi ya Sonko ya kugombea

6 Januari 2024

Baraza la Katiba la Senegal jana Ijumaa liliyakataa maombi ya kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko ya kugombea urais katika uchaguzi wa mwezi ujao.

https://p.dw.com/p/4av17
Kiongozi wa upinzani wa Senegal Ousmane Sonko
Kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara wa chama chake huko Dakar Juni 8, 2022. Sonko amezuiwa kuwania urais kwa madai kwamba baadhi ya nyaraka zake hazionekani Picha: Seyllou/AFP

Baraza hilo la Katiba la Senegal limesema kwamba baadhi ya nyaraka za Sonko hazionekani na ndio maana wamemzuia.

Mwanasheria wa Sonko Cire Cledor Ly, amesema baraza hilo hata hivyo halikufafanua zaidi lakini timu ya mawakili wake huenda ikawasilisha malalamiko mara baada ya kupata taarifa zaidi juu ya nyaraka hizo ambazo hazionekani.

Uamuzi huo ni pigo kubwa katika harakati zake za kugombea urais, ambazo tayari zimekumbwa na vizingiti kutokana na msururu wa kesi dhidi yake zilizoanzia na madai ya mwaka 2021.