1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani: Polisi watano washtakiwa kifo cha Msenegali

16 Februari 2023

Waendesha mashtaka nchini Ujerumani wamesema maafisa watano wa polisi wameshtakiwa kuhusiana na kifo cha kijana wa Kisenegali.

https://p.dw.com/p/4NY3Z
Deutschland Tagebau Garzweiler | Protest | Greta Thunberg, weggeführt von Polizei
Picha: Wolfgang Rattay/REUTERS

Kijana huyo mkimbizi aliyekuwa na umri wa miaka 16, alipigwa risasi na kuuawa na polisi mwaka uliopita.

Polisi inasema kijana alitishia kujidhuru kwa kisu kwenye nyumba ya kulea watoto mjini Dortmund.

Maafisa wanasema kijana huyo aliwakimbilia akiwa amebeba kisu, na kwamba walianza kumpulizia kemikali ya kuwasha kabla ya kutumia teza mbili, na baadae kumpiga risasi kwa kutumia bastola.

Soma pia:Verdi yaitisha mgomo Ujerumani wa kushinikiza masharti yao

Waendesha mashtaka wa mji wa Dortmund wamesema askari hao wa polisi walijibu kwa njia isiyo sawa, kulingana na vyombo vya habari vya Ujerumani.

Maafisa hao wa polisi hawakuwa na kamera za mwilini wakati wa ugomvi na kijana huyo wa Senegal.

Afisa wa polisi waUjerumani Gregor Lange amesema polisiwatahitaji kukabiliana na itikadi kali miongoni mwao kufuatia tukio hilo.

Tukio hilo lilizusha mjadala wa nchi nzima kuhusu mafunzo ya polisi na ubaguzi wa rangi.