1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mlinzi ubalozi Uingereza alituma taarifa 'nyeti' kwa Urusi

14 Februari 2023

Mlinzi wa zamani katika ubalozi wa Uingereza mjini Berlin anakabiliwa na kesi mjini London kwa kutoa mawasiliano ya "siri" ya serikali ya Uingereza kwa Urusi.

https://p.dw.com/p/4NRt6
Großbritannien London | Gerichtsverhandlung Pc David Carrick | PK
Picha: Jonathan Brady/empics/picture alliance

Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 58, anashtakiwa katika mahakama ya Old Bailey mjini London ambapo anatuhumiwa kukusanya taarifa nyeti kwa takribani miaka mitatu.

Waendesha mashtaka wanasema alituma barua mnamo Novemba 2020 ikiwa na taarifa kama hizo kwa afisa wa jeshi la Urusi.

Baada ya Uingereza, rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy akutana na Macron, Scholz mjini Paris

Ilikuwa na maelezo ya mawasiliano na anwani za wafanyakaziwa ubalozi, na pia anadaiwa kutoa mawasiliano ya siri na waziri mkuu wa zamani Boris Johnson na mawaziri wengine wandamizi wakati huo.

Mtuhumiwa huyo alikamatwa na afisa wa Uingereza aliejifanya kuwa mfanyakazi wa jeshi la Urusi, katika operesheni iliyoendeshwa kwa pamoja kati ya maafisa wa Ujerumani na Uingereza.