1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani kupeleka Kongo maabara ya kukabiliana na Mpox

21 Agosti 2024

Serikali ya Ujerumani imesema itapeleka maabara ya kuhamishika katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kusaidia kuwagundua wagonjwa wa homa ya Mpox na kudhibiti kuenea kwa maambukizi.

https://p.dw.com/p/4jka7
Kituo cha kutoa chanjo ya Mpox cha Bavaria
Kituo cha kutoa chanjo ya Mpox cha BavariaPicha: Sven Hoppe/dpa/picture alliance

Wizara ya Ushirikiano wa Kimaendeleo imesema leo kuwa pia kuna mipango ya kutoa mafunzo kwa wataalamu zaidi ili waweze kutambua dalili na kuufahamisha umma kuhusu hatua za kuzuia ugonjwa huo. Mafunzo sawa na hayo yaliandaliwa mwezi Juni mashariki mwa Kongo. Waziri wa Maendeleo wa Ujerumani, Svenja Schulze amesema maafisa wa Afrika wameomba msaada kutoka kwa jumuia ya kimataifa. Kulingana na Schulze, msaada huo unapaswa kutolewa.Wakati huo huo, Kongo imeripoti zaidi ya visa vipya 1,000 vya homa ya Mpox katika wiki iliyopita hadi kufikia jana. Visa hivyo vipya vimeripotiwa wakati ambapo maafisa wa afya barani Afrika wakiomba chanjo zinazohitajika kusaidia kupambana na kitisho kinachoongezeka cha ugonjwa hupo katika barani Afrika.