1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO: Mpox sio aina mpya ya UVIKO

20 Agosti 2024

Shirika la Afya Duniani WHO limetoa tamko rasmi leo Jumanne la kusisitiza kwamba ugonjwa wa homa ya nyani unaosababishwa na virusi vya mpox, sio ugonjwa mpya wa UVIKO unaosababishwa na virusi vya corona.

https://p.dw.com/p/4jhhK
Hans Kluge
Mkurugenzi wa WHO kanda ya Ulaya Hans Kluge asema jamii isidhani kwamba mpox ni aina mpya ya UVIKOPicha: Alberto Pizzoli/AFP/Getty Images

Tamko hilo limetolewa baada ya kuibuka kwa aina mpya ya kirusi cha clade 1 kinachosambaa kwa kasi barani Afrika na ambacho kimezusha wasiwasi kimataifa.

Mkurugenzi wa WHO kanda ya Ulaya Hans Kluge amewaambia waandishi wa Habari kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa kwamba inafaa kuishughulikia mpox kwa pamoja katika kuweka mifumo ili kuidhibiti na kuitokomeza kimataifa.

Msemaji wa shirika la afya duniani Tarik Jasarevic amesema WHO kwa sasa haijatoa mapendekezo ya watu kuvaa barakoa.