1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi wa Ujerumani kufanya kaguzi kuelekea Euro 2024

7 Juni 2024

Polisi wa Ujerumani huenda wakafanya ukaguzi wa muda kwenye mipaka yote ya nchi kuanzia leo Ijumaa wakati michuano ya Euro 2024 ikikaribia kuanza.

https://p.dw.com/p/4gl0z
Ujerumani, Stuttgart | EURO 2024
Polisi wakiwa kwenye zoezi la vitendo kwenye uwanja wa huko Stuttgart.Picha: Daniel Kubirski/picture-alliance

Waziri wa Mambo ya Ndani Nancy Faeser amesema hatua hiyo ni muhimu katika kuhakikisha ulinzi bora zaidi kwenye tukio hilo kubwa la kimataifa linalofanyika katika miji 10 ya Ujerumani.

Amesema, lengo ni kubaini na kuzuia uhalifu unaoweza kutokea katika siku za awali, kuanzia wa kigaidi hadi wa mitandaoni.

Polisi wa shirikisho watalinda mipaka ya Ujerumani, viwanja vya ndege na reli, wakati michuano hiyo ya Euro ikitarajiwa kuanza Juni 14 hadi fainali, Julai 14.