1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa Kenya watumbua upya makovu ya ufisadi

3 Agosti 2022

Uchaguzi mkuu nchini Kenya utakaofanyika Agosti 9, unayatumbua upya makovu ya ukosefu wa usawa na vilevile ufisadi. Wawaniaji wengi wa nyadhifa mbalimbali katika uchaguzi mkuu ujao nchini Kenya wametajwa kuwa mafisadi.

https://p.dw.com/p/4F4Lj
Mgombea urais wa muungano wa Kenya Kwanza William Ruto (kulia) na mgombea mwenza wake Rigathi Gachagua 8pili kulia) wakati wa mojawapo ya kampeni yao ya kwanza jijini Nairobi bJuni 4, 2022 baada ya kuidhinishwa na tume ya uchaguzi IEBC.
Mgombea urais wa muungano wa Kenya Kwanza William Ruto (kulia) na mgombea mwenza wake Rigathi Gachagua 8pili kulia) wakati wa mojawapo ya kampeni yao ya kwanza jijini Nairobi bJuni 4, 2022 baada ya kuidhinishwa na tume ya uchaguzi IEBC.Picha: Yasuyoshi Chiba/AFP

Waziri wa mambo ya ndani nchini humo Fred Matiangi ameeleza kwamba wagombea viti vya ubunge wanawahonga wapiga kura walioko vijijini kwa kuwapa hata shilingi 100 pekee kama njia ya kuwashawishi kuwapigia kura ili washinde kwenye uchaguzi huo.

Tume Huru ya Mipaka na Uchaguzi (IEBC) ambayo imefadhiliwa kidogo, lakini ambayo ilitaka kupunguza kiwango cha fedha ambazo wanaowania urais wanapaswa kutumia kwenye kampeni zao isipindukie bilioni 4.4, imewashutumu baadhi ya wanasiasa kwa kununua vitambulisho vya baadhi ya wananchi ili kuwazuia wasiwapigie kura washindani wao.

Si hayo tu, kati ya watu 214 walioorodheshwa na tume ya Maadili na kupambana na ufisadi kama waliokosa maadili na hawafai kuwa maafisa wa umma; tume ya uchaguzi iliwazuia sita pekee. Hayo yalisemwa mwezi Juni, na shirika la kupambana na ufisadi Transparency International na mashirika mengine yanayopambana na rushwa. Kuhusu wengine wote waliosalia kwenye orodha hiyo, tume ya IEBC ilishindwa kuwazuia. Juhudi zafanyika kuwazuia mafisadi kugombea nchini Kenya

Mgombea urais Raila Odinga (Kulia) wa muungano wa Azimio la Umoja na mgombea mwenza wake Martha Karua.
Mgombea urais Raila Odinga (Kulia) wa muungano wa Azimio la Umoja na mgombea mwenza wake Martha Karua.Picha: Yasuyoshi Chiba/AFP

Vita dhaifu dhidi ya ufisadi

Rais ambaye muhula wake madarakani unafikia ukingoni Uhuru Kenyatta, amekemea ufisadi na kutaka uwazi, lakini amefanya kidogo katika kuwezesha hilo katika muongo mmoja aliokuwa madarakani.

Wagombea wawili wakuu wa urais kwenye uchaguzi huo, naibu rais William Ruto mwenye umri wa miaka 55 wa chama cha muungano wa Kenya Kwanza, na Raila Odinga mwenye umri wa miaka 77 wa muungano wa Azimio la Umoja, wamesema watapambana na ufisadi. Lakini kulingana na mashirika yasiyo ya serikali yanayosikitishwa na hali ya Kenya kushindwa kuangamiza ufisadi unaoyaangamiza maisha ya raia kila siku, hizo zinasalia kuwa ahadi tu.

Nchini Kenya, wagombea viti vya kisiasa hawana ulazima kuweka bayana matumizi yao ya fedha za kampeni. Hata hivyo wananchi wameshuhudia wanasiasa wakitumia helikopta na misafara mirefu ya magari wakifanya kampeni nchi nzima kwa miezi kadhaa sasa.

Bango lenye picha ya mgombea urais wa chama cha Roots George Wajackoyah (kulia) akiwa na mgombea mwenza wake Justina Wamae kando ya mojawapo ya barabara za Nairobi.
Bango lenye picha ya mgombea urais wa chama cha Roots George Wajackoyah (kulia) akiwa na mgombea mwenza wake Justina Wamae kando ya mojawapo ya barabara za Nairobi.Picha: Yasuyoshi Chiba/AFP

Kenya: Viongozi watoa wito wa kuvumiliana kisiasa

Swali kuhusu vipi wanasiasa hufadhili kampeni zao

Timu za kampeni za Odinga na Ruto zilipoulizwa ni kiasi gani cha fedha wametumia kwenye kampeni zao, msemaji wa Odinga aliliambia shirika la habari la Associated Press kwamba watafanya hesabu mwishoni mwa kampeni ndipo wajue. Msemaji wa Ruto hakulijibu swali hilo.

Mara nyingi raia wa kawaida hubaki wakishangaa na kujiuliza swali gumu wasilojua la ni kiwango gani cha fedha wanasiasa wametumia kwenye kampeni zao kuelekea uchaguzi huo mkuu.

Martin Wambua ambaye huuza mitumba na ambaye mara nyingi humuwia vigumu kuweka hata akiba kidogo ya fedha, amedai bila kuwa na uhakika kwamba, wanasiasa hao hutumia mamilioni ya dola.

Kenya: Haki za binadamu zizingatiwe uchaguzi mkuu

Wachuuzi katika barabara kuu ya Outer Ring jijini Nairobi wameeleza kwamba wanalazimika kutoa hongo hospitalini ndipo waweze kuhudumiwa kwa wakati muafaka na kwamba wao huwahonga pia wakaguzi wa serikali ili kuepuka kukamatwa kwa madai ya makosa madogo madogo dhidi yao.

Mgombea urais David MWaure (katikati) wa chama cha Agano a,lipowasili kwenye ukumbi wa mdahalo ulioandaliwa baina ya wagombea urais Julai 26, 2022 jijini Nairobi.
Mgombea urais David MWaure (katikati) wa chama cha Agano a,lipowasili kwenye ukumbi wa mdahalo ulioandaliwa baina ya wagombea urais Julai 26, 2022 jijini Nairobi.Picha: John Ochieng/SOPA Images/ZUMAPRESS.com/picture alliance

Wanasiasa wahimizwa kuyakubali matokeo ya uchaguzi

Kwenye kivuli cha mojawapo ya mabango makubwa na mengi ya kisiasa yenye thamani kubwa ya pesa jijini Nairobi, wachuuzi wanajizatiti kuuza bidhaa zao ndipo wapate angalau shilingi 200 kwa siku. Siku nyingine wanakosa kuuza kabisa.

Ruto ashutumiwa kuanza harakati za kukataa matokeo ya uchaguzi

Na sasa wakati taifa hilo la Afrika mashariki lenye watu milioni 56 linapomtafuta mrithi wa Rais Uhuru Kenyatta, Wakenya wanahimiza uchaguzi wa amani na pande zote zikubali matokeo.

Andrew Atonya, mwanaharakati wa uchaguzi wa amani amesema ”tukipigana, sisi raia ndio tutaathiriwa zaidi wala si wanasiasa. Maana ukiwatizama wanasiasa wanatukanana hadharani, lakini nyuma ya pazia, wao ni marafiki”.

Ruto amesema atakubali matokeo ya uchaguzi huo. Vilevile Odinga amesema atakubali matokeo mradi tu uchaguzi uwe huru na wa haki.

(AP)