1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya: Haki za binadamu zizingatiwe uchaguzi mkuu

4 Julai 2022

Tume ya kutetea haki za binadamu nchini Kenya ilionesha wasiwasi kuhusu mauaji,unyanyasaji wa wanasiasa wanawake na ukiukwaji wa sheria unaoshuhudiwa kwa wakati huu wa kampeni, huenda yakadjhoofisha mchakato wa uchaguzi

https://p.dw.com/p/4De5m
Kenia Wahlwiederholung |  Unabhängige Wahlkommission (IEBC)
Picha: Reuters/T. Mukoya

Katika ripoti iliotolewa na tume hiyo ikiangalia masuala ya haki za binadamu kuelekea katika zoezi hilo muhimu la kikatiba, ilimulika  dhuluma dhidi ya wagombea wanawake wanaowania nyadhifa mbalimbali, kwenye uchaguzi huo wa Agasti.


Ripoti hiyo ambayo ilitolewa wakati kila mkenya akiwa makini katika kusikiliza sera za wagombea kwa ajili ya kufanya maamuziya kikatiba, ilimulika suala la usalama katika baadhi ya maeneo ya nchi.


Mwenyekiti wa tume hiyo  Roseline Odede,alisema watu wanne walipoteza maisha wakiwa katika mikutano ya kampeni za uchaguzi katika miji ambayo vuguvugu la kisiasa ni kubwa ikiwemo mji mkuu wa taifa hilo la Afrika Mashariki Nairobi, Kisii na Baringo.

Soma pia:Upotoshaji wa mtandaoni wachochea hofu Kenya kuelekea uchaguzi
Maeneo mengine ambayo ripoti hiyo ya tume ya haki za binadamu ilimulika hali ya usalama ni pamoja na  Lamu, Garissa, Marsabit, Elgeyo Marakwet, Nakuru, Mandera, Turkana na Pokot Magharibi.


Unyanyasaji wa kijinsia kwenye mchakato wa uchaguzi
Akiendelea kuelezea ripoti ilichabaini wakati taifa hilo linaelekea kwenye uchaguzi Mwenyekiti wa tume hiyo Odede alisema,wanasiasa wanawake ambao wameamua kujitosa kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi wamekuwa wakikumbana na kauli za kuudhi na kukatisha tamaa.

Kenia | Raila Odinga und in Nairobi
Matha Karua katikati Mgombea mwenza wa Raila OdingaPicha: Raila Odinga press Team

Aidha aliongeza kuwa hatua hiyo ilizusha wasiwasi kwa miongoni mwa wagombea na wafuasi wao, hatua aliotazamwa kama ni ukiukwaji wa sheria na kanuni za uchaguzi Kenya ilizojiwekea katika kufanikisha zoezi hilo la kikatiba.


"Tumepokea visa vya unyanyasaji wakati wa mchujo ndani ya vyama vya siasa" Alisema Odede wakati akiwasilisha ripoti hiyo kwa umma na kuongeza kuwa matukio hayo yanaendelea kushuhudiwa hata wakati huu wa kampeni.


Alimulika namna majukwaa ya mitandao ya kijamii yanavyotumiwa kisiasa katika kudhoofisha nia za wanasiasa wanawake kuendelea kuwania nafasi za uwakilishi wa wananchi katuika vyombo vya maamuzi.

Soma pia:Uidhinishwaji wagombea wa uchaguzi Kenya wakamilika


"Visa hivi ni pamoja na mitandao ya kijamii,mashambulizi ya kimwili" alisema mwenyekiti huo huku akisisitiza kuwa tume haitavumia unyanyasaji huo katika kipindi hiki muhimu kwa taifa.


Tume hiyo imetambua kwamba Kenya itakuwa inafanya uchaguzi wa tatu chini ya katiba mpya ya mwaka 2010 bila utaratibu mwafaka wa namna ya kuhakikisha sheria ya thuluthi mbili ya jinsia inatekelezwa.


Kushirikisha watoto wakati wa kampeni za uchaguzi
Wakitoa ripoti ya hali ya haki za kibinadamu kwenye kipindi hiki cha uchaguzi, tume hiyo ilionesha namna ambavyo baadhi ya shule zilikatiza shughuli za masomo kwenye baadhi ya maeneo na wananfunzi ambao wengi ni chini ya umri wa miaka 18, kuruhusiwa kushiriki katika mikutano ya kisiasa.


Baadhi ya shule ziliwatoa wanafunzi darasani na kwenda kuwaimbia wanasiasa ikiwa ni sehemu ya kuchangamsha mikutano ya kampeni na hata kushangilia hoja za wanasiasa wanaosaka kura.

Feiertag in Kenia I Mashujaa Day I Symbolbild
Wananchi wakiwa kwenye mkusanyiko wa pamoja KenyaPicha: Dai Kurokawa/epa/dpa/picture alliance


Aidha tume hiyo ambayo imeendelea kumulika utekelezwaji wa haki za binadamu na sheria wakati huu wa uchaguzi ilinakiri matukio 47 ya matumizi ya rasilimali za umma wakati huu wa kampeni za uchaguzi.


"Tunapinga hatua hii sio haki kwa wagombea wengine" Alisema mmoja wa ofisa wa tume hiyo ya haki za binadamu na kuongeza kuwa wagombea wote wana haki sawa kwa mujibu wa sheria.

Mchakato wa kuwahamisha wapiga kura uangaliwe upya
Tume hiyo vilevile ilisema kuna zoezi la kuwahamisha watu linaloendelea, kwa hiari au pasipo hiari, hatua ambayo walitaja huenda likatatiza mchakato wa upigaji kura.


Katika kzufuatilia mchakato huo wa uhamishaji wapigta kura wamekariri visa 149 ya ushawishi wa wapiga kura.  
Tume ya uchaguzi ya Kenya, IEBC ilithibitisha kuyaondoa majina ya wapiga kura  takriban laki tano, kutoka kwenye sajili yao ya wapiga kura.

Soma pia:Tume ya IEBC Kenya yafanyia majaribio mfumo wake wa matokeo
Wakati zikiwa zimesalia takriaban siku 36 kufanyika kwa zoezi hilo la kikatiba, tume hiyo ilisema wapiga kura hao wameoondolewa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo, makosa ya usajili wa mara zaidi ya moja.


Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati alimesa tume hiyo imejidhatiti kuhakikisha inaendesha zoezi hilo la kidemocrasia kwa weledi wa hali ya juu.


“Tuko tayari kuwahudumia wananchi wa taiaf hili. Hiyo ni ahadi tunatoa.”


IEBC ieleze mikakati yake kuelekea uchaguzi mkuu
Kufuatia ripoti waliyoiwasilisha, tume ya Kenya ya kutetea kaki za binadamu inaitaka tume ya uchaguzi na mipaka Kenya IEBC, kuelezea bayana mikakati iliyowekwa kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa huru na wa haki.


Imesema mikakati hiyo itasaidia washiriki wote katika zoezi hilo la kikatiba kushiriki kwa kutambua haki na wajibu wao,kwenye matokeo ya kurejesha imani ya Wakenya kwenye mchakato huo.

Juhudi za amani kabla ya uchaguzi Kenya