1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tunisia yawalazimisha mamia ya wahamiaji kuondoka

13 Julai 2023

Shirika la Hilali Nyekundu limesema zaidi ya wahamiaji 600 waliolazimishwa kuondoka katika bandari ya Sfax ya Tunisia hadi kwenye maeneo ya mpakani mwa Libya wanahifadhiwa na kupewa misaada ya kibinadamu.

https://p.dw.com/p/4TqtO
Tunesien | Ausschreitungen in Sfax, Migranten
Picha: REUTERS

Mamia ya wahamiaji kutoka mataifa ya Afrika iliyo kusini mwa jangwa la Sahara, walikimbia au kulazimishwa kuondoka Sfax kufuatia ghasia za ubaguzi wa rangi.

Ghasia hizo zilizuka kufuatia mauaji ya kijana wa Tunisia mnamo Julai 3 wakati wa makabiliano kati ya wenyeji na wahamiaji.

Soma zaidi: Miili ya wahamiaji yapatikana kwenye mpaka wa Tunisia-Algeria
HRW yaitaka Tunisia kuacha kuwafurusha wahamiaji wa Kiafrika

Wengi wa wale waliofukuzwa kutoka Sfax waliachwa katika jangwa karibu na mipaka ya Tunisia ambapo walikabiliwa na hali mbaya.

Sfax ni eneo kuu linalotumiwa na wahamiaji wengi wanaoondoka kutoka mataifa maskini na yale yaliyokumbwa na machafuko, kwa matumaini ya kutafuta maisha bora barani Ulaya.