1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miili ya wahamiaji yapatikana mpaka wa Tunisia-Algeria

12 Julai 2023

Miili ya wahamiaji wawili imepatikana kwenye eneo la jangwa karibu na mpaka wa Tunisia na Algeria, siku kadhaa tangu kuzuka uhasama baina ya wenyeji na wageni kwenye mji wa mwambao wa Tunisia wa Sfax

https://p.dw.com/p/4Tlh0
Tunesien | Ausschreitungen in Sfax, Migranten
Picha: HOUSSEM ZOUARI/AFP

Hayo yameelezwa na afisa mmoja wa mahakama na shahidi mwingine aliyekata kutambulishwa jina lake kwa sababu za usalama. Kulingana na msemaji wa mahakama ya wilaya ya Tozeur ya kusini mashariki mwa Tunisia, mwili wa kwanza ulipatikana siku 10 zilizopita kwenye jangwa la Hazoua na mwili mwingine ulipatikana Jumatatu ya wiki hii.

Soma pia: Wahamiaji 300 hawajulikani waliko baharini Atlantiki

Afisa huyo amesema mamlaka zimefungua uchunguzi wa "kifo cha mashaka" ili kubaini sababu za watu hao waiwli kupoteza maisha.

Wahamiaji kutoka mataifa ya kusini mwa jangwa la Sahara waliokuwa wakiishi kwenye mji wa Sfax wametumbukia kwenye uhasama na wenyeji baada ya kifo cha mwanaume mmoja raia wa Tunisia kilichotokea Julai 3. Mwanaume huyo alidungwa kisu wakati wa makabiliano kati ya pande hizo mbili.

Tangu wakati huo mamia ya wahamiaji wamelazishwa kuukimbia mji huo wa wamesafirishwa kwa nguvu na kupelekwa kwenye eneo la Jangwa kwenye mpaka wa Tunisia na mataifa jirani ya Algeria na Libya.