1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

THE HAGUE: Kesi ya mauaji ya Srebrenica yafunguliwa tena

21 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDJP

Kesi ya maafisa saba wa Bosnia wenye asili ya Kiserb imeanza tena mjini The Hague.Maafisa hao wameshtakiwa kuhusika na mauaji ya yaliotokea Srebrenica.Muendesha mashtaka wa Umoja wa Mataifa,Carla Del Ponte amesema washtakiwa hao saba ni miongoni mwa wale waliohusika zaidi na mauaji ya wanaume na watoto wa kiume wa kiislamu wapatao takriban 8,000.Mauaji hayo yalitokea Julai mwaka 1995 katika mji wa mashariki wa Bosnia,Srebrenica.Mbali na mauaji ya halaiki,watu hao 7 wameshtakiwa pia makosa yanayohusika na maangamizi.Alipoifungua kesi,Del Ponte alisema ni jambo lisiloweza kusamehewa kuwa Serbia imekataa kumtoa Ratko Mladic,ambae ni mshukiwa mkuu kuhisika na ukatili huo.