1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Suu Kyi ahukumiwa miaka 5 jela kwa ufisadi

Hawa Bihoga
27 Aprili 2022

Mahakama ya kijeshi nchini Myanmar imemtia hatiani kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Aung San Suu Kyi kwa ufisadi na kumuhukumu kifungo cha miaka mitano jela.

https://p.dw.com/p/4AUwO
Myanmar | Win Htein
Picha: AFP/Getty Images

Adhabu hiyo imekosolewa vikali na wafuasi wake na wataalamu wa masuala ya sheria ambao wanasema imelenga kumuondoa kiongozi huyo wa kiraia kwenye ulingo wa kisiasa.

Suu Kyi ambae aliondolewa madarakanina utawala wa kijeshi mwezi February mwaka uliopita alikanusha madai kwamba alipokea dhahabu na maelfu ya dola kama hongo kutoka kutoka kwa mwanasiasa mwenzake wa ngazi za juu ambae ni waziri mkuu wa Yangon. adhabu ya juu kutokana na kosa hilo ni kifungo cha miaka 15 jela pamoja na faini.

Wafuasi wake na wataalamu huru wa sheria walikosoa vikali mashataka hayo ambayo wameyataja kuwa si ya haki na yalimaanisha kumuondoa Suu Kyi mwenye umri wa miaka 76 kwenye ulingo wa siasa.

Tayari alikuwa amehukumiwa kifungo cha miaka 6 katika kesi nyingine iliokuwa ikimkabili ikiwemo kukiuka kanuni za kudhibiti maambuikizi ya Corona.

Soma zaidi:Korti ya kijeshi kutoa uamuzi katika kesi ya Suu Kyi

Mwanaharakati Wai Hnin Pwint Thon alilaani hukumu hiyo iliomtia hatiani kuiongozi huyo na kusema imechochewa kisiasa.

Aliyataja kuwa hayo ni nashata ya uongo na yalichochekwa kisiasa, lakini mkumfunga kiongozi huyo kwa kipindi kirefu ni kumuweka mbali kwenye ulingo wa kisiasa.

"wanajeshi wanafikiria kwa kumuhukumu wanaondoa matumaini kwa watu. Lakini kiuhalisia ipo kinyume" alisema mwanaharakati huyo huku akisisitiza kuwa watu hawajapoteza matuamaini bado wanaupinga utawala wa kijeshi.

Wanahabari,wafuasi wazuiliwa kuhudhuria kesi hiyo

Habari za uamuzi huo zilizolewa na afisa wa sheria ambae ambae alioomba kutotajwa jina lake kwa sababu hana mamalaka ya kutoa taarfa.

Myanmar Yangon | Proteste gegen Militärregime an Geburtstag von Aung San Suu Kyi
Wafuasi wa Aung San Suu Kyi wakiwa mtaani kupinga kufunguliwa kesi kwa kiongozui huyoPicha: AFP

Kesi ya kionongozi huyo ilioondeshwa katika mji mkuu wa Naypaytaw waandishi wa habari na wafuasiwake walizuiwa kuhudhuria huku wanasheria wake wakipigwa marufuku kuzungumza na vyombo vya habari.

Soma zaidi:Kiongozi wa kijeshi Myanmar aapa kuwaangamiza wanamgambo

Haijajulikana kama kiongozi huyo atatumikia kifungo cha  gerezani au atakuwa kwenye kizuizi cha nyumbani.

Suu Kyi alikamatwa Februari1 mwaka jana, saa chache kabla ya tukio hilo lilipindua kiongozi wa kiraia aliechaguliwa kidemocrasia na kurudisha taifa hilo lililopo kusini mashariki mwa bara la  Asia kwenye utawala wa kijeshi

Machafuko yameendelea kushuhudiwa tangu jeshi lilipofanya mapinduzi

Myanmar imekuwa katika machafuko ya kisiasa tangu mapinduzi ya kijeshi, na wanajeshi wakijitahidi kuzuia maandamano ya amani yanayofanywa na raia mitaani kupinga utawala wa kijeshi.

Symbolbild Widerstandskämpfer in Myanmar
Askari wakizuia maandamano ya kiraia kupinga utawala wa kijeshi MyanmatPicha: Aung Kyaw Htet/SOPA Images/ZUMA Wire/picture alliance

Makundi yenye silaha ambayo yanasaidiwa na wapinzani wa utawala huo yakiendeleza harakati zake ili kuung'oa utawala huo.

Soma zaidi:Mwaka mmoja wa mapinduzi ya kijeshi Myanmar waadhimishwa kwa maandamano

Kulingana na chama cha kusaidia wafungwa wa kisiasa wamerekodi visa vya mauaji na ukiukwaji wa haki za binadamu takriban watu 1700 waliuwawa huku zaidi ya 130000 wakikamatwa tangu taifa hilo kushuhudia mapinduzi ya kijeshi mwaka uliopita.