1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Sudan yageuka uwanja wa mapigano kwa wapiganaji wa kigeni

15 Mei 2023

Wataalam wasema Sudan imekuwa uwanja wa mapigano kwa wapiganaji kutoka nje, pamoja na washirika wanaoliunga jeshi ambao wanavutiwa na fedha pamoja na dhahabu za nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4RNMG
Sudan Proteste und Kämpfe in Khartoum
Picha: AFP

Kwa muda mrefu, Sudan ilikuwa ikiwatuma mamluki kupigana nchi za nje. Lakini kwa sasa, nchi hiyo ndiyo imegeuka uwanja wa mapambano wa mamluki kutoka nje.

Mwakilishi waalum wa Umoja wa Mataifa Volker Perthes, amesema wapiganaji wanaotaka kujitajirisha na mali ya Sudan, wanamiminika katika nchi hiyo kutoka pande mbalimbali za Afrika ikiwemo nchi za ukanda wa Sahel kama Mali, Chad na Niger.

Wanamgambo wa RSF walishutumu jeshi kushambulia hospitali

Perthes ametahadharisha kwamba idadi ya wapiganaji hao wa kigeni si ndogo.

Mkuu wa majeshi ya Sudan Abdel Fattah al-Burhan amewashutumu mahasimu wake wa kikosi cha wanamgambo Rapid Support (RSF), kwa kuwasajili wapiganaji kutoka mataifa jirani wakiwemo mamluki kutoka Chad, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Niger.

Je RSF linawasajili wapiganaji wa kigeni?

Jeshi la Sudan limedai kumuua mlenga shabaha wa kigeni ambaye ni miongoni mwa wakuu wa wanamgambo wa RSF.

Mashuhuda mjini Khartoum pia wamesema wamesikia baadhi ya wanamgambo wa RSF wakizungumza Kifaransa, lugha ambayo hutumika katika taifa jirani la Chad.

Kwa muda wa mwezi mmoja sasa, Sudan imekumbwa na mapigano makali kati ya Burhan, mkuu wa jeshi la taifa hilo na Mohamed Hamdan Daglo, mkuu wa wanamgambo wa RSF.

Vita vya Sudan vyatinga mwezi bila matumaini ya kumalizika

Katika miaka ya hivi karibuni, bunduki za kundi la RSF zimekuwa zikikodishwa na kutumika na muungano w akijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia katika vita vya Yemen, dhidi ya waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran.

Jenerali Abdulfattah al-Burhan anayeliongoza jeshi la Sudan alituhumu kundi la RSF kuwasajili wapiganaji wa kigeni.
Jenerali Abdulfattah al-Burhan anayeliongoza jeshi la Sudan alituhumu kundi la RSF kuwasajili wapiganaji wa kigeni.Picha: Sudan Sovereignty Council Press Office/AA/picture alliance

Aidha kundi hilo limekuwa likipeleka wapiganaji wake kuunga mkono pande mbalimbali katika machafuko ya Libya, ukiwemo upande wa Jenerali wa mashariki ya Libya Khalifa Haftar.

Marekani na Umoja wa Ulaya zililishutumu kundi la RSF kuwa na mafungamano na kampuni ya wapiganaji binafsi kutoka Urusi Wagner. Kundi ambalo linapigana nchini Ukraine kwa sasa, lakini ambalo pia limekuwa likituma wapiganaji wake katika machfuko kadhaa ya Afrika ikiwemo Libya.

Hivi karibuni, mkuu wa kampuni ya Wagner Yevgeny Prigozhin alisistiza kuwa kwa miaka miwili, hakuna mpiganaji hata mmoja wao ambaye amekuwa akipigana nchini Sudan n ahata sasa hakuna yeyote.

Lakini Cameron Hudson ambaye ni mtaalam wa masuala ya kivita katika kituo cha Kimkakati na masomo ya Kimataifa alisema, Wagner hawapigani Sudan, lakini kampuni hiyo ina washauri wake wa kiufundi nchini Sudan.

Mashambulizi yaendelea Khartoum wakati wapinzani wakikutana Saudia

Mnamno Februari, Umoja wa Ulaya uliiwekea Wagner vikwazo, huku ukiishutumu kwa kukiuka haki za binadamu nchini Ukraine na vilevile Sudan, Mali na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Wachambuzi wadai washauri wa kivita wa Wagner wako Sudan

Wakati vita vya Sudan vilipoanza Aprili 15, Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken alielezea wasiwasi wake mwingi kuhusu kuhusika kwa kampuni ya Wagner kwenye machafuko hayo. Aliishutumu Wagner kwa kusababisha vifo na uharibifu mwingi popote inaposhiriki mapigano.

Wanadiplomasia wan chi za Magharibi wameripoti kuyaona makundi ya mamluki yakipitia uwanja wa ndege wa Khartoum na kwenye hoteli za Khartoum, tangu serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati ilipowaalika wapiganaji wa Wagner kuisadia kupapambana na uasi.

Kwa muda mrefu familia ya Daglo imekuwa ikidhibiti machimbo ya dhahabu eneo la Darfur na kwingineko nchini Sudan, taifa la tatu ulimwenguni kwa uzalishaji wa kito hicho cha thamani ambacho kimeivutia kampuni ya Wagner.

Wizara ya fedha ya Marekani imemshutumu Prighozin kwa kuendesha kampuni vivuli nchini Sudan ambazo zilipewa kandarasi za uchimbaji dhahabu.

Kundi la RSF lilianzia wanamgambo wa Janjaweed waliohangaisha vijiji vya Darfur tangu mwaka 2003, ambapo walidaiwa kufanya maovu mengi na uhalifu wa kivita.
Kundi la RSF lilianzia wanamgambo wa Janjaweed waliohangaisha vijiji vya Darfur tangu mwaka 2003, ambapo walidaiwa kufanya maovu mengi na uhalifu wa kivita.Picha: MOHAMMADKHAIR ABDUALRHMAN/REUTERS

Vikwazo vya hivi karibuni vya Umoja wa Ulaya vinalenga kampuni za dhahabu zinazohusishwa na kundi la Wagner nchini Sudan.

Andreas Krieg, professa mwandamizi wa somo la usalama katika chuo cha Kings mjini London amesema kwa Daglo, dhahabu imekuwa chanzo chake cha fedha kuwalipa wapiganaji.

Krieg ameliambia shirika la habari la AFP, kwamba maadamu Daglo ana utajiri mkubwa wa dhahabu, anaweza kulipa mishahara kwa namna ambayo nchi nyingi za kusini mwa janga la Sahara au Sahel haziwezi.

Udhibiti wa machimbo ya dhahabu wampa Dagalo uwezo wa kifedha

Hivi karibuni, kwenye ukurasa wao mmoja wa kijamii wanamgambo wa RSF walichapisha video ilioonesha wapiganaji wakiwa Chad na Niger na kuwaunga mkono.

Ingawa RSF huweza kupata wapiganaji kutoka Chad na kwingineko, wachambuzi wanasema inaaminika kwamba wanapata silaha kutoka Libya hasa kutoka kwa waasi wanaoongozwa na Khalifa.  

Mchambuzi wa Sudan Alex Waal amesema pes ana wapiganaji vimekuwa vitu vya kubadilishana katika siasa za Sudan na Daglo anashiriki biashara hiyo.

Kwenye uchambuzi wake wa hivi karibuni, Waal aliandika kwamba RSF ni biashara binafsi ya mamluki wa nchi mbalimbali.

(Chanzo: AFPE)