1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi yaendelea Khartoum, wapinzani wakikutana Saudia

13 Mei 2023

Mashambulizi ya anga yameshuhudiwa Jumamosi kwenye mji mkuu wa Sudan, Khartoum, huku wawakilishi wa pande hasimu wakikutana Jeddah, Saudi Arabia kwa mazungumzo ya kuzuia janga la kibinaadamu.

https://p.dw.com/p/4RJ7p
Sudan Khartum | Kämpfe, Rauch
Picha: Ahmed Satti/Anadolu Agency/picture alliance

Mtu aliyeshuhudia ameripoti kuhusu mashambulizi ya anga ya jeshi dhidi ya kikosi maalum cha wanamgambo wa RSF, wakati mashambulizi hayo yakiingia wiki yake ya tano.

Zaidi ya watu 750 wameuawa na maelfu wameyakimbia makaazi yao kutokana na mapigano ya kuwania madaraka kati ya Mkuu wa Majeshi, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na msaidizi wake, kamanda wa RSF Mohamed Hamdan Daglo.

Soma zaidi:UNHCR:Takriban watu 200,000 kutoka Sudan wamekimbilia nchi jirani

Siku ya Alhamisi, wawakilishi wa pande zinazohasimiana nchini Sudan walikubaliana kuhusu mpango wa kuwalinda raia na kuruhusu upelekwaji wa misaada ya kiutu, ingawa mapigano bado yanaendelea.

Mazungumzo ya kesho yataangazia jinsi ya kutekeleza makubaliano hayo na kuwaondoa wanajeshi kutoka kwenye maeneo ya raia.