1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz azuru Korea Kusini, baada ya mkutano wa G7 Japan

22 Mei 2023

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz ameonya kuhusu majaribio ya makombora ya nyuklia na masafa marefu yanayofanywa na Korea Kaskazini.

https://p.dw.com/p/4ReVh
Südkorea | Bundeskanzler Besuch Olaf Scholz in Seoul
Picha: Chung Sung-Jun/Getty Images

Hayo ni wakati Ujerumani na Korea Kusini zikiajiandaa kusaini makubaliano ya kuimarisha ushirikiano wa ulinzi. Rais wa Korea Kusini Yoon Suk-yeol alitangaza jana muafaka huo wakati wa ziara ya Scholz mjini Seoul.

Alisema unalenga kuzilinda siri za kijeshi na kusaidia kuendesha kwa urahisi ugavi wa sekta ya ulinzi. Scholz alisema majaribio ya makombora ya Korea Kaskazini ni ishara ya "hali bado kuwa hatari" kwenye rasi ya Korea.

Soma pia: Kansela wa Ujerumani Scholz kuhudhuria mkutano wa G7 Ijumaa

Scholz alizuru Korea Kusini jana, baada ya kuhudhuria mkutao wa kilele wa G7 mjini Hiroshima, Japan. Ndiye Kansela wa kwanza wa Ujerumani kuzuru mji mkuu wa Korea Kusini kwa mkutano wa pande mbili katika kipindi cha miaka 30.