1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela wa Ujerumani Scholz kuhudhuria mkutano wa G7 Ijumaa

20 Februari 2023

Kansela wa Ujerumani, Olaf Scholz anatarajia kuhudhuria mkutano wa viongozi wa kundi la nchi saba tajiri duniani, G7, utakaofanyika siku ya Ijumaa.

https://p.dw.com/p/4Nl4v
Belgien Brüssel | EU-Gipfel | Olaf Scholz
Picha: John Thys/AFP

Mkutano huo utakaokuwa kwa njia ya mtandao, unafanyika katika siku ya kukumbuka mwaka mmoja tangu Urusi ilipoivamia Ukraine, Februari 24.

Wakati huo huo, Scholz anatarajiwa kukutana na Rais wa Marekani Joe Biden Machi 3 mwaka huu.

Msemaji wa serikali ya Ujerumani, Steffen Hebestreit amesema mkutano kati ya viongozi hao wawili utafanyika nchini Marekani.

Alipoulizwa ikiwa ziara hiyo imeratibiwa mahsusi ili Ujerumani na Marekani ziweze kuratibu utoaji zaidi wa silaha kwa Ukraine, Hebestreit amesema mazungumzo hayo ni yanayoendelea na hayatokuwa ajenda kuu katika ziara hiyo ya mwezi Machi.