1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Schily ana matumaini kuhusu sheria mpya ya uhamiaji.

17 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFrk
NÜRNBERG: Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani Otto Schily anatazamia kwamba Halmashauri ya Uwiyano katika bunge la Ujerumani itaweza kuwafikiana hapo mwakani juu ya sheria mpya ya uhamiaji. Sheria hiyo mpya ya uhamiaji inahitajiwa haraka ili kuyatenganisha maswali ya uhamiaji na maombi ya himaya ya kisiasa, alisema mwanasiasa huyo wa chama tawala cha SPD, kufuatana na sherehe za kuadhimishwa mwaka wa 50 tangu iundwe afisi kuu ya wakimbizi wa kigeni mjini Nuremberg. Wakati huo huo, Waziri huyu wa Mambo ya Ndani alitoa mwito wa kuwiyanishwa siasa ya wakimbizi ya UU.