1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ripoti: Mwezi Julai ulivunja rekodi ya kuwa na joto kali

8 Agosti 2023

Ripoti mpya baada ya kukamilika uchunguzi wa mabadiliko ya hali ya hewa barani Ulaya inaonesha kuwa mwezi wa Julai ulikuwa ni mwezi wenye kiwango cha juu zaidi cha joto kilichowahi kuorodheshwa duniani.

https://p.dw.com/p/4UvIU
Joto kali
Mkazi wa Ugiriki akijaribu kujipoza kwa chupa ya majiPicha: Louisa Gouliamaki/AFP/Getty Images

Ripoti mpya baada ya kukamilika uchunguzi wa mabadiliko ya hali ya hewa barani Ulaya uliofanywa  taasisi ya Umoja wa Ulaya ya Copernicus inayoshughulikia maswala ya Mabadiliko ya Tabianchi inaonesha kuwa mwezi wa Julai ulikuwa ni mwezi wenye kiwango cha juu zaidi cha jotokilichowahi kuorodheshwa duniani.

Ripoti hiyo imeeleza kwamba ongezeko la joto la nyuzi joto 0.33,liilipindukia kiwango cha mwezi Julai, mwaka 2019 cha wastani wa nyuzi joto 0.72.  Naibu mkurugenzi wa Taasisi ya Copernicus Samantha Burgess amesema siku ya Julai 6 ndio ilikuwa ya joto zaidi duniani hadi kufikia sasa.