1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia wa Australia wanaozuiliwa syria wataka warejeshwe kwao

26 Septemba 2023

Zaidi ya wanawake 30 wa Australia na watoto wanaoishi katika "hali mbaya" kwenye kambi walikozuiliwa nchini Syria, leo wamefunguwa kesi mahakamani kuilazimisha Canberra kuwarudisha nyumbani.

https://p.dw.com/p/4Wok5
Askari jeshi akiwa katika doria kwenye moja ya miji ya Syria
Picha: Samya Kullab/AP/picture alliance

Kesi inayohusu suala hili ilifunguliwa katika mahakama kuu ya mjini Melbourne takriban mwaka mmoja baada ya Australia kuwarudisha nyumbani kutoka Syria, wanawake wengine wanne na watoto 13 likiwa ni kundi la mwisho la familia za waliokuwa wapiganaji wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu.

Soma pia:Mjumbe wa UN nchini Syria awasihi wafadhili wasisitishe misaada

Shirika la msaada la Save the Children linaloshughulikia suala hilo limesema serikali ya Australia imeshindwa katika jukumu lake la kuwarejesha salama nyumbani raia wake wote kutoka Syria.

Shirika hilo limeiomba mahakama kutowa kibali kinachoonesha raia wa Australia wanazuiliwakinyume cha sheria katika kambi ya Al Roj nchini Syria, na hivyo kuilazimisha serikali kuwarejesha nyumbani watu hao.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW