1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yatangaza 'ushirikiano wa kimkakati' na Syria

22 Septemba 2023

Rais wa China Xi Jinping ametangaza kile alichokiita kuwa ni “ushirikiano wa kimkakati” kati ya nchi yake na Syria alipokutana na rais Bashar al Assad.

https://p.dw.com/p/4WhbK
China | Xi Jinping na Bashar al-Assad
Rais Xi Jinping wa China akutana na Rais Bashar al-Assad wa Syria mashariki mwa mji wa HangzhouPicha: SANA/REUTERS

Xi amesema hayo wakati wa mazungumzo na rais wa Syria Bashar al-Assad anayetafuta msaada wa kifedha kusaidia kuijenga upya nchi yake iliyoharibiwa na machafuko.

Kulingana na taarifa iliyosomwa na shirika la habari linalomilikiwa na China CCTV, Xi alisema ushirikiano huo utakuwa hatua muhimu katika historia ya uhusiano wa nchi hizo mbili, lakini bila ya kutoa maelezo zaidi.

Viongozi hao wamekutana katika mkesha wa sherehe za ufunguzi wa michezo ya bara la Asia, ambayo Assad atahudhuria kama sehemu ya ziara yake ya kwanza nchini China tangu mwaka 2004.