1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mjumbe wa UN Syria awasihi wafadhili wasisitishe misaada

10 Septemba 2023

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Geir Pedersen ametoa wito kwa wafadhili wasipunguze misaada nchini humo wakati mgogoro wa kiuchumi ukizidi kuongezeka.

https://p.dw.com/p/4WAS0
Geir O. Pedersen, UN-Sondergesandter für Syrien
Picha: Martial Trezzini/picture alliance/KEYSTONE

 Akizungumza na waandishi wa habari mjini Damascus, Pedersen amesema hali ya uchumi ndani ya Syria imezidi kuwa mbaya kuliko wakati mzozo ulipokuwa umepamba moto nchini humo.

Soma pia: UN yasema imeafikiana na Syria kuhusu uingizaji misaada

Itakumbukwa kuwa, Rais wa taifa hilo, Bashar al Assad, aliongeza kiwango sha mishahara mara mbili kwa wafanyakazi wa sekta ya umma na pensheni mwezi uliopita, hali iliyoongeza mfumuko wa bei na kuchochea maandamano yanayoendelea ambayo yalitikisa mikoa ya Sweida na karibu na mji wa Dara.

Kutokana na hali ngumu ya  uchumi raia wenye hasira, walitaka Assad ajiuzulu, wito sawa na wa mwaka 2011 uliosababisha maandamano yaliyogeuka kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimeingia katika mwaka wa 13 sasa.