1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS. Amri ya kutotoka nje nchini Ufaransa

9 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEK7

Ufaransa imetangaza hali ya hatari ambayo itawalazimu watu wasitoke majumbani mwao katika miji kadhaa nchini humo kufuatia machafuko ya wiki mbili zilizopita yaliyosababisha vifo na kuharibiwa kwa mali za watu.

Habari zaidi kutoka Paris zinaeleza kwamba hali imeanza kuwa tulivu ijapokuwa ghasia ziliendelea kwa uchache kufikia jana usiku.

Takriban watu 70 wamekamatwa, mamia ya magari kuchomwa na maduka kuporwa.

Utawala wa Ufaransa umesema ghasia hizo ziliwahusisha vijana wenye asili ya kifaransa, vijana wazaliwa wa ufaransa wenye asili ya kiarabu au ya kiafrika ambao wanapinga ubaguzi wa rangi na ukosefu wa kazi miongoni mwao.