1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nagelsmann atumai Rudiger atacheza dhidi ya Denmark

29 Juni 2024

Duru ya mtoano ya mashindano ya kandanda ya ubingwa wa Ulaya - UEFA Euro 2024 yanayofanyika hapa Ujerumani inaanza Jumamosi ambapo mechi mbili zitachezwa.

https://p.dw.com/p/4hens
Mashindano ya Euro 2024
Kikosi cha Ujerumani kiliwasili Dortmund tayari kuvaana na Denmark katika mechi ya duru ya 16 za mwishoPicha: Bernd Thissen/dpa/picture alliance

Ujerumani itakabana koo na Denmark mjini Dortmund katika mechi ya usiku ikiwa na matumaini kuwa beki wa kati Antonio Rudiger atajumuishwa kikosini. Beki huyo mwenye umri wa miaka 31 alirejea mazoezini Ijumaa kufuatia jeraha la paja alilopata katika mechi waliyotoka sare ya 1 - 1 na Uswisi wakati Ujerumani ilimaliza kama kinara wa Kundi A.

Soma pia: Euro 2024: Timu 16 zajipanga katika hatua ya mchujo

Kocha wa Ujerumani Julian Nagelsmann amesema madaktari wamefanya kila wawezalo kuhakikisha kuwa yuko sawa kurudi uwanjani. Rudiger huenda akashirikiana katika safu ya ulinzi na Nico Schlotterbeck, ambaye atachukua nafasi ya Jonathan Tah anayetumikia adhabu ya kadi za njano. Katika ushambuliaji, Nagelsmann alikataa kufichua ni nani atakayeanza kati ya Kai Havertz na Niclas Füllkrug.

Katika mechi ya mapema jioni, Uswisi itashuka dimbani dhidi ya mabingwa watetezi Italia. Kocha wa Uswisi Murat Yakin amesema anatumai kusababisha mshangao dhidi ya Wataliano mjini Berlin.