1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Germany yafuzu kwa duru ya mtoano kombe la EURO

Josephat Charo
20 Juni 2024

Kocha wa Ujerumani Julian Nagelsmann amesema mashabiki sasa wanaweza kuota ndoto ya kwenda Berlin kushudia fainali.

https://p.dw.com/p/4hHLT
Wachezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani
Wachezaji wa timu ya taifa ya UjerumaniPicha: Angelika Warmuth/REUTERS

Wenyeji Ujerumani imekuwa timu ya kwanza kufuzu kwa duru ya mtoano ya michuano ya kombe la EURO 2024 baada ya kuichapa Hungary 2-0 kupitia mabao ya Jamal Musiala na nahodha Ilkay Gundogan katika mbungi kali ya kundi A iliyochezwa katika dimba la MHP Arena mjini Stuttgart.

Hungary sasa inakabiliwa na kibarua kigumu ikitarajia kucheza mechi yake ya mwisho ya kundi A dhidi ya Scotland Jumapili ijayo, ambayo ilitoka sare 1-1 na Uswisi hapo jana. Ujerumani wao watakuwa na miadi na Uswisi mechi yao ya mwiho ya makundi.

Leo Slovenia itakwaana na Serbia huku Denmark ikiwa na miadi na England katika mechi za kundi C. Baadaye mabingwa watetezi wa kombe la EURO Italia watanyukana na Uhispania katika pambano la kundi B. Kocha wa Uhispania Luis de la Fuente anaiona mbungi hiyo kuwa muhimu zaidi hadi sasa na ni mechi ya maamuzi na fainali ya mapema.