1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIndia

Modi aapishwa kuwa Waziri Mkuu India kwa muhula wa tatu

9 Juni 2024

Narendra Modi ameapishwa leo kwa muhula wa nadra wa tatu mfululizo kama Waziri Mkuu wa India.

https://p.dw.com/p/4gqS8
India | Narendra Modi
Narendra Modi, kulia, akisalimiana na Rais wa India, Droupadi Murmu, baada ya kuapishwa kuwa Waziri Mkuu wa India kwenye ukumbi wa Rashtrapati Bhawan, New Delhi, India, Jumapili, Juni 9, 2024. Picha: Manish Swarup/AP Photo/picture alliance

Modi alitegemea washirika wake wa muungano baada ya chama chake kushindwa kupata wingi wa viti bungeni katika matokeo ambayo hayakutarajiwa.

Modi na Baraza lake la mawaziri walikupa kiapo, kilichosimamiwa na Rais Droupadi Murmi, katika kasri la rais la Rashtrapati Bhavan mjini New Delhi.

Soma pia: Mpinzani wa Modi ateuliwa kuongoza kambi ya upinzani bungeni

Waziri Mkuu huyo mwenye umri wa miaka 73 ambaye ni maarufu lakini anayesababisha mgawanyiko ndiye waziri mkuu wa pili pekee wa India baada ya Jawaharlal Nehru kubakia madarakani kwa muhula wa tatu wenye miaka mitano.

Chama chake cha siasa kali za kizalendo cha Bharatiya Janata - BJP, ambacho kilishinda kwa kishindo katika uchaguzi wa 2014 na 2019, kilishindwa kupata wingi wa viti ili kuunda serikali kivyake katika uchaguzi wa karibuni wa kitaifa.

Hata hivyo, muungano wa Modi wa National Democratic Alliance ulishinda viti vya kutosha kuunda serikali ikiongozwa naye.