1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mpinzani wa Modi kuongoza kambi ya upinzani bungeni

Sylvia Mwehozi
8 Juni 2024

Mwanasiasa wa chama cha Congress Rahul Gandhi ambaye ni mpinzani mkuu wa Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, ameteuliwa kuongoza kambi ya upinzani bungeni baada ya kumalizika kwa uchaguzi nchini humo.

https://p.dw.com/p/4gosL
Indien I Rahul Gandhi - Congress
Mwanasiasa wa chama cha Congress Rahul Gandhi Picha: Altaf Qadri/AP/picture alliance

Mwanasiasa wa chama cha Congress Rahul Gandhi ambaye ni mpinzani mkuu wa Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, ameteuliwa kuongoza kambi ya upinzani bungeni baada ya kumalizika kwa uchaguzi nchini humo.Modi atarajiwa kukutana na washirika kujadili kuunda serikali

Gandhi ameteuliwa katika mkutano mkuu wa chama cha Congress uliofanyika leo Jumamosi, na kuidhinishwa kwa kauli moja kama kiongozi rasmi wa upinzani nchini India, nafasi ambayo ilikuwa imeachwa wazi tangu mwaka 2014.

Chama cha Gandhi cha Congress kimeongeza viti vyake bungeni mara mbili ikiwa ni matokeo mazuri tangu Modi alipoingia mamlakani.

Waziri Mkuu Modi anatarajiwa kuapishwa rasmi mwishoni mwa juma hili kwa muhula wa tatu madarakani, kufuatia matokeo ya uchaguzi ambayo yalikinyimachama chake tawala cha BJP wingi wa viti bungeni na hivyo kutazamiwa kushirikiana na vyama vingine kuunda serikali.