1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Modi kukutana na washirika kujadili kuunda serikali

5 Juni 2024

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi anatarajiwa leo kukutana na washirika wake kujadili kuunda serikali, siku moja baada ya chama chake cha Bharatiya Janata (BJP) kupoteza wingi wa viti bungeni.

https://p.dw.com/p/4gfEP
Indien Mumbai 2024 | Premierminister Narendra Modi bei Wahlkampfveranstaltung
Waziri Mkuu wa India na kiongozi wa chama tawala cha Bharatiya Janata Party (BJP) Narendra Modi (katikati) akiwa na waziri mkuu wa jimbo la Maharashtra Eknath Shinde (kushoto) na naibu wao mkuu Devendra Fadnavis (kulia) akipungia mkono Mumbai. Mei 15, 2024.Picha: Punit Paranjpe/AFP/Getty Images

Matokeo rasmi ya uchaguzi huo yaliyotangazwa jana jioni, yameonesha kuwa BJP kilishinda viti 240 pekee katika uchaguzi huo mkuu, kukiwa na upungufu wa viti 32 kufikia nusu ya idadi ya viti katika bunge jilo lenye wajumbe 543. Matokeo hayo yamewashtua wawekezaji na kusababisha hisa kushuka kwa kasi, kwani Modi atalazimika kutegemea vyama vyengine vya majimbo kuunda serikali, na ambavyo kuaminika kwao kisiasa kumeyumba. Lakini juhudi zozote za kuunda serikali na upinzani huenda zimezuiliwa na washirika wawili wakuu wa BJP waliomuidhinisha Modi na kusema muungano wao wa kabla ya uchaguzi na chama hicho ulikuwa thabiti.