1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Mkuu wa genge la uhalifu Ecuador ahamishiwa jela nyingine

13 Agosti 2023

Ecuador imemhamisha kiongozi mwenye nguvu wa genge la uhalifu, anayetuhumiwa kumtishia mgombea urais kabla ya kuuawa.

https://p.dw.com/p/4V70o
Ecuador Guayaquil | Polizeieinsatz in Hochsicherheits Gefängnis
Picha: Vicente Gaibor Del Pino/REUTERS

Kwenye saa za alfajiri, karibu maafisa 4,000 waliokuwa na silaha nzito waliingia gereza namba 8 katika mji wa Guayiaquil, kusini magharibi mwa Ecuador, ambako kiongozi wa kundi la uhalifu la Los Choneros, Jose Adolfo Macias, almaarufu Fito, alikuwa anashikiliwa tangu mwaka wa 2011.

Soma pia: Marekani kusaidia uchunguzi mauaji ya mgombea urais Ecuador

Rais wa Ecuador Guillermo Lasso alitangaza kwenye mtandao wa X kuwa Fito alipelekwa katika gereza la La Roca. Ecuador imekuwa chini ya hali ya hatari tangu tukio la kushtusha la kuuliwa mwandishi habari aliyegeuka kuwa mwanasiasa Fernando Villavicenzio.

Mgombea huyo aliyekuwa na umri wa miaka 59 alipigwa risasi wakati akiondoka katika mkutano wa kampeni katika mji mkuu Quito. Wiki moja kabla ya kuuliwa, alisema Fito alikuwa akimtishia. Chama chake kimesema mgombea mwenza wake Andrea Gonzalez atachukua nafasi yake katika uchaguzi huo wa Agosti 20.