1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaEcuador

Marekani kusaidia uchunguzi mauaji ya mgombea urais Ecuador

11 Agosti 2023

Rais wa Ecuador Guillermo Lasso amesema ameliomba Shirika la Upelelezi la Marekani, FBI kusaidia katika uchunguzi wa mauaji ya mgombea wa urais, Fernando Villavicencio.

https://p.dw.com/p/4V2VN
Mgombea urais Ecuador auwawa
Mgombea urais nchini Ecuador Fernando Villavicencio aliuwawa kwa kupigwa risasi siku ya Jumatano, Agosti, 9, 2023.Picha: ASSOCIATED PRESS/picture alliance

Lasso amesema FBI imekubali ombi lao na maafisa wake watawasili Ecuador muda wowote kuanzia leo.

Villavicencio, aliyekuwa mgombea wa upinzani, aliuawa kwa kupigwa risasi siku ya Jumatano wakati akitoka kwenye kampeni kwenye mji mkuu, Quito.

Takribani watu wengine tisa walijeruhiwa. Watu sita walikamatwa jana usiku nchini Ecuador, wakihusishwa na mauaji ya Villavicencio.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Juan Zapata, ameyaelezea mauaji hayo kama uhalifu wa kisiasa wenye mazingira ya kigaidi, ambayo yana lengo la kuhujumu uchaguzi wa Agosti 20.