SiasaEcuador
Mgombea urais nchini Ecuador auawa kwa kupigwa risasi
10 Agosti 2023Matangazo
Taarifa hiyo imetolewa na rais Rais wa Ecuador Guillermo Lasso aliyesema kuwa kitendo hicho kitaadhibiwa.
Villavicencio mwenye umri wa miaka 59 na mwenye watoto watano, alikuwa mmoja wa wagombea wanane katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Agosti 20 mwaka huu na alikuwa mwanachama wa Vuguvugu lenye dhamira ya Kuijenga Ecuador.
Alikuwa pia mkosoaji mkubwa dhidi ya ufisadi hasa wakati wa serikali ya Rais wa zamani Rafael Correa kuanzia mwaka 2007 hadi 2017.
Mauaji hayo yanajiri huku kukiwa na wimbi la ghasia katika taifa hilo la Amerika ya Kusini, linaloshuhudia pia ongezeko la biashara ya dawa za kulevya na mauaji ya kikatili.