1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Mgombea mwenye msimamo wa wastani kileleni uchaguzi wa Iran

29 Juni 2024

Mgombea asiye maarufu mwenye msimamo wa wastani anaongoza katika matokeo ya uchaguzi wa mapema wa urais nchini Iran kati ya kikundi cha wagombea wanne wanaomtii kiongozi mkuu Ayatollah Ali Khamenei.

https://p.dw.com/p/4henw
Wagombea katika uchaguzi wa Iran
Wagombea sita waliidhinishwa kushiriki uchaguzi wa Iran lakini wawili wakajiondoa kinyang'anyironiPicha: Shafaqna

Huku zaidi ya kura milioni 3.8 zikiwa zimehesabiwa hadi sasa, Massoud Pezeshkian anaongoza na zaidi ya kura milioni 1,595,000 na mpinzani wake wa msimamo mkali, mpatanishi wa zamani wa mazungumzo ya nyuklia Saeed Jalili akiwa na karibu milioni 1,594,000. Hayo yametangazwa kwenye televisheni na afisa wa wizara ya mamho ya ndani Mohsen Eslami.

Vyanzo vinasema idadi ya wapiga kura waliojitokezailikuwa karibu asilimia 40, ikiwa ni chini kuliko ilivyotarajiwa na watawala wa kidini wa Iran. Shirika la habari la Iran, Tasnim, limesema kuna uwezekano mkubwa wa uchaguzi huo kuingia duru ya pili ili kumpata mrithi wa Ebrahim Raisi aliyekufa katika mkasa wa kuanguka helikopta.

Soma pia: Rais wa Iran amefariki katika ajali ya helikopta

Uchaguzi huo unafanyika sanjari na kuongezeka kwa mvutano wa kikanda kutokana na vita kati ya Israel na washirika wa Iran Hamas huko Gaza na Hezbollah nchini Lebanon, pamoja na kuongezeka kwa shinikizo la Magharibi kwa Iran kuhusu mpango wake wa nyuklia unaoendelea kwa kasi.