1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Iran afariki katika ajali ya helikopta

20 Mei 2024

Rais wa Iran Ebrahim Raisi, Waziri wake wa Mambo ya Nchi za Nje Hossein Amir-Abdollahian na maafisa wengine, wamepatikana wamekufa katika eneo la ajali ya Helikopta iliotokea hapo jana.

https://p.dw.com/p/4g47w
Tehran, Iran | Aliyekuwa Rais wa Iran Ebrahim Raisi enzi za uhai wake
Aliyekuwa Rais wa Iran Ebrahim Raisi enzi za uhai wake akihutubia maadhimisho ya miaka 45 Mapinduzi ya Kiislamu yaliyofanyika mjini Tehran Februari 11, 2024.Picha: Iran's Presidency/WANA/Handout via REUTERS

Miili ya viongozi hao pamoja na maafisa wake imepatikana baaada ya saa nzima ya kuwatafuta katika eneo la milima lililokuwa na ukungu mwingi Kaskazini Magharibi mwa   Iran. 

Shirika la habari la Iran bado hadi sasa halijatoa chanzo  cha ajali hiyo.

Ebrahim rais aliyeaga dunia akiwa na miaka 63, amekuwepo madarakani tangu mwaka 2021 wakati Iran ikikumbwa na maadamano makubwa dhidi ya serikali, mgogoro wa kiuchumi uliozidi kuiathiri nchi hiyo  hasaa baada ya Marekani kuiwekea vikwazo, pamoja na mvutano uliopo kati yake na adui yake wa muda mrefu Israel. 

Soma pia:Rais wa Iran aripotiwa kufa katika ajali ya helikopta

Hapo jana Jumapili kiongozi wa juu wa taifa hilo Ayatollah Ali Khamenei aliwatolea wito raia wa Iran kuwa watulivu na kutokuwa  na wasiwasi juu ya uongozi wa Jamhuri hiyo ya kiislamu. 

Taarifa zinasema tayari kiongozi wa juu zaidi wa Iran,Khamenei ametangaza siku tano za maombolezo ya kitaifa na amemtangaza Mohammad Mokhber kukaimu nafasi ya rais. Mokhber, aliye na miaka 68, alikuwa makamu wa rais.