1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia wa Iran wanapiga kura leo kumchagua rais mpya

28 Juni 2024

Raia wa Iran wanapiga kura leo kumchagua rais mpya kufuatia kifo cha Rais Ebrahim Raisi kilichotokea kutokana na ajali ya helikopta zaidi ya mwezi mmoja uliopita.

https://p.dw.com/p/4hd11
Iran | Mgombea wa nafasi ya urais Mohammad Bagher Ghalibaf akipiga kura.
Mgombea wa nafasi ya urais Iran Mohammad Bagher Ghalibaf akipiga kura.Picha: Majid Asgaripour/WANA/REUTERS

Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa kuanzia saa mbili asubuhi saa za Iran na vinatarajiwa kufungwa saa kumi na mbili jioni japo zoezi hilo linaweza kuendelea hadi saa sita za usiku.

Uchaguzi huo ulioandaliwa kwa haraka unatokea katikakati ya mvutano wa kikanda juu ya mzozo kati ya Israel na Hamas, pamoja na ongezeko la shinikizo kutoka mataifa ya Magharibi kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.

Soma pia: Wairan waelekea vituoni kumchagua rais mpya kumrithi Raisi

Wachambuzi wameeleza kuwa, matokeo ya uchaguzi wa leo hayawezi kuleta mabadiliko makubwa katika sera za Jamhuri hiyo ya Kiislamu lakini yanaweza kuamua ni nani atakayemrithi kiongozi mkuu wa kidini Ayatollah Ali Khamenei, aliyekuwa madarakani tangu mwaka 1989.