1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Melenchon aikemea Rwanda kujitanua Kongo

27 Oktoba 2023

Kiongozi wa msimamo mkali wa mrengo wa kushoto nchini Ufaransa Jean-Luc Melenchon amekemea kile alichokiita "malengo ya kujitanua" Rwanda mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://p.dw.com/p/4Y6Et
Kiongozi wa mrengo wa kushoto Ufaransa Jean-Luc Melenchon
Kiongozi wa mrengo wa kushoto Ufaransa Jean-Luc Melenchon Picha: Nasser Berzane/abaca/picture alliance

Hayo ni wakati mapigano yakipamba moto kati ya waasi na makundi ya wapiganaji yanayoiunga mkono serikali.

Akizungumza baada ya kukutana na Rais Felix Tshisekedi wa Kongo, Melenchon alisema alitaka kusisitizaudugu wake na watu wa Kongo, katika wakati ambapo wanakabiliwa na changamoto ambayo inasababishwa na nchi nyingine.

Uchaguzi mkuu wa Kongo unatarajiwa Disemba 20, na Tshisekedi ni mmoja wa wagombea.

Soma pia:Mapigano mapya yazuka mashariki ya Congo

Watalaamu huru wa Umoja wa Mataifa, Kongo pamoja na Ufaransa na Marekani zinaituhumuRwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 ambao wamekamata maeneo makubwa ya mashariki mwa Kongo tangu mwaka wa 2021.

Hapo jana, waasi hao walifanya mashambulizi mapya kaskazini mwa mji wa Goma, huku mapigano kati yao na makundi yanayoiunga mkono serikali yakiendelea kusambaa hadi kusini.