1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Mashirika makubwa ya ndege yafuta safari kuelekea Tel Aviv

9 Oktoba 2023

Mashirika makubwa ya ndege yamefuta safari zao kuelekea katika mji mkuu wa Israel, Tel Aviv wikendi hii iliyomalizika, kufuatia shambulio la Hamas dhidi ya Israel

https://p.dw.com/p/4XH4M
Vikosi vya ulinzi wa raia vya Palestina vyajaribu kuzima moto katika nyumba iliyoteketezwa na shambulizi la anga la Israel huko Khan Younis, Kusini mwa Ukanda wa Gaza, Jumapili Oktoba 8, 2023
Vikosi vya ulinzi wa raia vya Palestina, vyazima moto uliosababishwa na mashambulizi ya anga ya Israel Picha: Yousef Masoud/AP/picture alliance

American Airlines, Air France, Lufthansa, Emirates na Ryanair ni miongoni mwa mashirika hayo yaliyositisha safari katika uwanja wa ndege wa Ben Gurion.

Huduma za kibiashara zaendelea katika uwanja wa Eilat

Hata hivyo, mamlaka za viwanja vya ndege  hazijasimamisha huduma za kibiashara na uwanja wa pili wa kimataifa nchini Israel wa Eilat ambao ni kituo cha watalii kwenye Bahari ya Sham.

Soma pia:Watu wasiopungua 40 wameuawa Israel katika mashambulizi ya Hamas

Israel imetangaza vita rasmi dhidi ya kundi la Hamas, ambapo waziri mkuu Benjamin Netanyahu ameapa kufika katika kila kona linakopatikana kundi hilo la wanamgambo wa Kipalestina.