1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Urusi yailenga miundombinu ya nishati nchini Ukraine

Sylvia Mwehozi
22 Juni 2024

Ukraine imesema leo kwamba Urusi imefanya mashambulizi makubwa ya usiku kucha na kuilenga miundombinu ya nishati upande wa magharibi na mashariki mwa nchi.

https://p.dw.com/p/4hNwk
Ukraine | Ukrenergo
Miundombinu ya shirika la ugavi wa umeme la UkrainePicha: Ukrainische nationale Energiegesellschaft „Ukrenergo“

Ukraine imesema leo kwamba Urusi imefanya mashambulizi makubwa ya usiku kucha na kuilenga miundombinu ya nishatiupande wa magharibi na mashariki mwa nchi. Taarifa iliyotolewa na wizara ya nishati ya Ukraine ilisema kuwa mashambulizi hayo yameharibu vifaa vya shirika la ugavi wa umeme la Ukrenergo kwenye mikoa ya Zaporizhzhia na Lviv na kujeruhi wafanyakazi wawili.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amekaririwa akisema kuwa mashambulizi ya Urusi yameharibu nusu ya uwezo wa miundombinu ya nishati nchini humo. Kiongozi huyo alinukuliwa mapema wiki hii akisema kuwa hospitali na shule nchini Ukraine zitapaswa kufungwa vifaa vya Sola haraka iwezekanavyo.Ukraine yakabiliwa na matatizo ya umeme kufuatia mashambulizi ya Urusi

Mashambulizi ya Urusi ya makombora na Droni yametatiza uwezo wa uzalishaji wa umeme wa Ukraine na kuilazimu Kyiv kuanzisha mgao wa umeme na uagizaji wa bidhaa kutoka Umoja wa Ulaya.