1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maashambulizi ya anga yaendelea Sudan

12 Mei 2023

Mashambulizi ya anga na makombora yameendelea katika mji mkuu wa Sudan Khartoum leo Ijumaa baada ya pande mbili zinazovutana kushindwa kukubaliana kusitisha mapigano

https://p.dw.com/p/4RGYh
Sudan Khartum Kämpfe Bürgerkrieg
Picha: Mohamed Nureldin/REUTERS

Jeshi rasmi la serikali na wanamgambo wa RSF wameshindwa kukubaliana kusitisha mapigano licha ya kuahidi kuwalinda raia na kuruhusu kupisha misaada ya kibinadamu. Kile kilichoitwa tamko la kanuni za makubaliano kilisainiwa jana jioni  mjini Jeddah nchini Saudi Arabia baada ya mazungumzo ya takriban wiki moja kati ya pande hizo mbili, ingawa hakuna upande hata mmoja ambao mpaka sasa umetowa taarifa ya kuyatambuwa makubaliano hayo. Makubaliano hayo yaliyosainiwa jana yametokana na mazungumzo yaliyosimamiwa na Saudi Arabia na Marekani  na yanajumuisha ahadi za pande zote mbili kuruhusu  raia, wataalamu wa afya, na misaada ya kibinadamu  pamoja na kupunguza madhara kwa raia na majengo ya umma.