1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin atulia, magharibi waztunguka

10 Januari 2022

Rais wa Urusi Vladimir Putin anafurahia wakati msururu wa mikutano ya ngazi ya juu kuhusu usalama barani Ulaya ikianza wiki hii. Ni wakati bora kwa mtawala wa kiimla kama huyu, anasema mwandishi wa DW Bernd Riegert.

https://p.dw.com/p/45M2P
Russland Präsident Wladimir Putin
Picha: Mikhail Metzel/Sputnik/Kremlin Pool Photo via AP/picture alliance

Vladimir Putin lazima atakuwa mwenye furaha wakati akijiandaa kwa diplomasia na wiki nzima kati ya Kremlin na mataifa ya magharibi. Mkururo wa mikutano ya maafisa wa ngazi ya juu na wakuu wa nchi na serikali imepangwa mjini Geneva, Brussels, Vienna na Brest, Ufaransa, yote ikiwa na lengo moja: Kumfurahisha rais wa Urusi na kuepusha uvamizi unaohofiwa wa Urusi dhidi ya Ukraine.

Harakati hizo za kidiplomasia zilianza mnamo mwezi Desemba kwa simu mbili za mazungumzo kati ya marais wa Marekani na Urusi. Mazungumzo hayo yalifuatiwa na mkutano wa vidio wa mawaziri wa mambo ya nje wa jumuiya siku ya Ijumaa, ambamo msimamo wa magharibi kuhusu Urusi uliwekwa wazi.

Deutsche Welle Hintergrund Deutschland Bernd Riegert
Mwandishi wa DW mjini Brussels, Bernd RiegertPicha: DW

Rais wa Marekani Joe Biden ameahidi kushauriana kwa karibu na washirika wa Ulaya kuhusu suala hilo, na amekariri maneno yake. Jana Jumatatu, wawakilishi wa juu wa Marekani wamefanya mazungumzo ya kimkakati na ujumbe wa Urusi mjini Geneva.

NATO yatafakari kinachofuata

Siku ya Jumatano kutakuwa na mkutano mjini Brussels wa Baraza la NATO na Urusi, jukwaa la mashauriano ambalo halijakutana kwa miaka kadhaa. Na wakati huo huo, wakuu wa majeshi wa NATO watakutana kuzingatia uimarishaji wa vikosi vya muungano huo kwenye Bahari Nyeusi, au mpaka wa mashariki wa NATO.

Soma pia: Umoja wa Ulaya kujadili kuhusu mkutano wa kilele na Putin

Siku ya Alhamisi, mazungumzo yataendelea katika mfumo mpana wa shirika la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya, lenye makao yake mjini Vienna, Austria, yanayozihusisha Marekani pamoja na Urusi, Ukraine na mataifa mengine ya zamani ya Kisovieti.

Umoja wa Ulaya pia, umedhamiria kutoachwa nje. Mawaziri wa ulinzi na mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya watakutana katika mji wa Ufaransa wa Brest siku za Jumatano, Alhamisi na Ijumaa. Kama ilivyo kwa mikutano yote mingine iliyopangwa, mada kuu kwenye ajenda itakuwa matakwa ya Urusi ya uhakikisho wa kiusalama na hatuza zinazoweza kuchukuliwa iwapo Putin ataivamia Ukraine.

EU yawekwa kando katika usalama wa Ulaya

Kikubwa cha kuondoka nacho ni kwamba rais wa Urusi ameweza kuyachanganya mataifa ya magharibi, na kudhihirishwa wazi mitazamo inayokinzana katika kambi pinzani. Inapokuja kwenye uhusiano na Urusi, kuna tofauti za wazi ndani ya NATO na Umoja wa Ulaya kutegemeana na maslahi ya mataifa wanachama.

Ukraine Luhansk-Region | Josep Borrell, EU
Mkuu wa sera ya nje wa EU Josep Borrell ambaye hivi karibuni nchini Ukraine amelalamika Umoja wa Ulaya kuwekwa kando.Picha: Andriy Dubchak/AP Photo/picture alliance

Mkuu wa sera ya kigeni wa Umoja wa Ulaya Joseph Borrell, amelalamika hata kwamba kanda hiyo imeachwa nje -- alisema hata hakuulizwa - linapokuja suala la usalama barani Ulaya na Ukraine. Hii leo, Ulaya haijaweza kukubaliana juu ya hasa vikwazo gani vikali wanataka kutumia kuitisha Urusi.

Soma pia: Umoja wa Ulaya washindwa kukubaliana mkutano na Putin

Kitu kimoja tu EU imeamua ni kwamba Moscow laazina ilipe gharama kubwa iwapo itachochea uhasama wake dhidi ya Ukraine.

Muafaka kwa ajili ya Kremlin

EU inasita kwa namna inayoeleweka, kulenga sekta itakayoiumiza vibaya Urusi, ambayo ni ugavi wa nishati. Bila mafuta na gesi kutoka Urusi, mataifa kadhaa barani Ulaya, ikiwemo Ujerumani, yatakuwa katika matatizo makubwa. Putin yumkin hatashughulikia maazimio yoyote mazito yanayochukuliwa wakati wa wiki hii kali ya diplomasia.

Inawezekana kwamba ataona maonyo sawa ambayo yamekuwa yakitolewa tangu 2014, wakati Urusi ilipopeleka kwa mara ya kwanza majeshi yake kwenye mpaka wa mashariki mwa Ukraine.

Putin na Biden wakutana

Siyo Marekani wala mataifa ya NATO yatapeleka majeshi yao kuisaidia Ukraine. Na inasalia kuwa vigumu kwamba NATO itakubali takwa la Moscow kwamba NATO izikatalie uanachama Ukraine na Georgia. Mataifa ya magharibi hayatokubali vitisho vya Urusi, na Putin analijua hilo vyema.

Soma pia: Armin Laschet: Kwa Urusi 'unapaswa kuzungumza zaidi, siyo kidogo'

Lakini Biden tayari ameihakikishia Kremlin kwamba uanachama wa Georgia na Ukraine ndani ya NATO hauko kwenye ajenda kwa wakati ujao, hali kama hii imekuwepo tangu mkutano wa kilele wa NATO wa mwaka 2008 mjini Bucharest.

Mataifa ya Magharibi yataendelea kutumia ushawishi, yakitegemea diplomasia katika juhudi za kutochokoza hatua za kijeshi za Urusi. Na Putin ataendelea kuyatia kiwewe mataifa ya magharibi kwa uchokozi wake wa maksudi.