Le Pen, washirika wake wapandishwa kizimbani kwa ubadhirifu
30 Septemba 2024Matangazo
Tuhuma hizo zinawahusu wasaidizi wa bunge wa chama cha Le Pen kuanzia mwaka 2004 hadi mwaka 2016.
Wengi wao hawakuweza kuyafafanua majukumu yao ya kila siku na wengine hawakuwahi kukutana na wakubwa wao wa kazi au hata kukanyaga majengo ya bunge.
Soma zaidi: Macron afanya mazungumzo na Le Pen kuhusu Waziri Mkuu
Kosa la ubadhirifu wa fedha za umma linaadhibiwa kwa faini ya hadi Euro milioni1.1 au kifungo cha miaka 10 jela.
Huenda kesi hiyo ikamwathiri Le Pen anayetumai kujaribu kugombea urais nchini Ufaransa kwa mara ya nne mnamo mwaka 2027.