1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Macron afanya mazungumzo na Le Pen kuhusu Waziri Mkuu

26 Agosti 2024

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amekutana na kiongozi wa siasa kali za mrengo wa kulia Marine Le Pen kwa mazungumzo ya nadra hii leo.

https://p.dw.com/p/4jvDl
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa. Picha: Ludovic Marin/AFP/dpa/picture alliance

Mkutano wao umefanyika katika wakati shinikizo likizidi kumtaka ateue waziri mkuu baada ya uchaguzi wa bunge wa Julai ambao haukutoa mshindi wa moja kwa moja.

Le Pen pamoja na wanachama wa chama chake cha National Rally waliingia Ikulu ya Elysee bila ya shamrashamra yoyote kabla ya mkutano huo, ingawa Rais Macron hakuonekana.

Tangu Alhamisi, Macron aliwaalika viongozi wa vyama vya siasa huko Elysee kwa matumaini ya kupata mgombea asiyetiliwa shaka na pande zote.

Uchaguzi wa mapema ulioitishwa na Macron mwezi uliopita ulishindwa kuiondoa Ufaransa kutoka kwenye mkwamo wa bunge ambao ulishuhudia kambi yake ikiongoza serikali ya walio wachache tangu 2022.