1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Korea Kusini yasitisha mkataba wa kijeshi na Korea Kaskazini

22 Novemba 2023

Korea Kusini imesitisha sehemu ya mkataba wa kijeshi iliyousaini Korea Kaskazini mwaka 2018, baada ya Pyongyang kupuuza tahadhari zilizotolewa na Marekani na kudai imefanikiwa kutuma angani satelaiti ya upelelezi.

https://p.dw.com/p/4ZItn
Meli ya kivita ya Marekani na mshirika wake Korea Kusini
Meli ya kivita ya Marekani na mshirika wake Korea KusiniPicha: Yonhap via REUTERS

Hatua hiyo ya kusitisha kipengele katika makubaliano hayo, itashuhudia Korea Kusini ikiongeza doria za kijeshi katika mpaka wa nchi hizo.

Makubaliano hayo ambayo yalikuwa yananuiakupunguza mivutano kati ya nchi hizo mbiliyalisainiwa mwaka 2018 kati ya rais wa zamani wa Korea Kusini Moon Jae-in na Kim Jong Un.

Soma pia:Marekani na Korea Kusini zarekebisha makubaliano ya kuikabili Korea Kaskazini

Korea Kusini na Japan ambazo ndizo nchi za kwanza kuripoti uzinduzi wa setlaiti hiyo, haizikuweza kuthibitisha mara moja iwapo setlaiti hiyo ilikuwa katika mzunguko wa dunia. Wizara ya ulinzi ya Marekani imesema jeshi lake bado linachunguza iwapo uzinduzi huo ulifanikiwa.