1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kusini

Korea Kusini kurusha satelaiti yake ya kwanza ya ujasusi

6 Novemba 2023

Korea Kusini imesema inapanga kurusha mwishoni mwa mwezi huu, setellite yake ya kwanza iliyoundwa nchini humo,ili kuifuatilia vizuri Korea Kaskazini ambaye ni hasimu wake.

https://p.dw.com/p/4YSA1
Vifaru vya kijeshi vya Korea Kusini vikiwa katika gwaride la jeshi
Vifaru vya kijeshi vya Korea Kusini vikiwa katika gwaride la jeshiPicha: Ahn Young-joon/AP Photo/picture alliance

Mpango huo wa Korea Kusini unafanyika katika wakati ambapo jirani yake huyo wa Kaskazini  anaendelea kutanuwa uwezo wake wa silaha za Kinyuklia kuwalenga maadui zake. 

Msemaji wa  wizara ya ulinzi ya Korea Kaskazini,Jeon Ha Gyu amewaambia waandishi habari leo Jumatatu kwamba setalaiti ya kwanza ya kijeshi ya ujasusi  itarushwa kutoka kambi ya jeshi la wanaanga ya Vandenberg,huko Carlifonia Marekani Novemba 30. 

Soma pia:Korea Kusini, Marekani na Japan wailaani Korea Kaskazini

Korea Kusini imekuwa  ikitegemea setellite za ujasusi za Marekani kuchunguza mienendo ya Korea Kaskazini.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW