1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani na Korea Kusini zaboresha makubaliano ya kijeshi

13 Novemba 2023

Mawaziri wa Marekani na Korea Kusini wameboresha makubaliano yao muhimu ya kijeshi dhidi ya Korea Kaskazini, hii ikiwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha muongo mmoja.

https://p.dw.com/p/4YjlO
Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin
Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin Picha: Johanna Geron/REUTERS

Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin yuko mjini Seoul kushiriki mkutano wa mwaka wa usalama pamoja na mwenzake wa Korea Kusini Shin Won-sik, wakati washirika hao wakiimarisha ushirikiano wa kiulinzi katikati ya ongezeko la vitisho vya makombora na nyuklia kutoka Pyongyang.

"Tumejaribiwa kila wakati, na tumedhibiti kila changamoto. Kwa pamoja, tulijenga mojawapo ya ushirikiano imara zaidi na wenye uwezo mkubwa ulimwenguni. Tumezuia migogoro na uchokozi mkubwa kwenye Rasi ya Korea kwa miongo saba. Ni muhimu, na tutaendelea kuwa tayari kupambana," alisema Austin.

Korea Kaskazini imesema inachokifanya Marekani ni kuchochea wasiwasi wa kisiasa na kijeshi katika Rasi ya Korea

Kulingana na taarifa, mabadiliko kwenye makubaliano hayo yaliyofikiwa mwaka 2013 yanamaanisha, kuanzia sasa yataruhusu washirika hao kuzuia kwa ufanisi zaidi hatua za Korea Kaskazini za kuendeleza mipango yake ya nyuklia na isiyo ya nyuklia yenye athari za kimkakati.