1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Korea Kusini yahairisha kutuma satelaiti ya kijasusi

28 Novemba 2023

Korea Kusini yaahirisha mipango yake ya kutuma satelaiti ya kijasusi katika mzingo wa dunia.

https://p.dw.com/p/4ZWZr
Korea Kaskazini | Satilaiti ikipaa kuelekea kwenye mzingo wa dunia
Satilaiti ya Korea Kaskazini ikiruka kuelekea katika mzingo wa dunia.Picha: KCNAvia REUTERS

Korea Kusini imeahirisha mipango yake ya kutuma satelaiti yake ya kwanza ya kijasusi katika mzingo wa dunia, siku chache tu baada ya hasimu wake Korea Kaskazini kurusha satelaiti yake ya kijasusi kwa mara ya kwanza.

Chini ya mkataba wa SpaceX, Korea Kusini ilitarajiwa kutuma satelaiti tano za kijasusi katika mzingo wa dunia kufikia mwaka 2025 na urushaji wake wa kwanza ulikuwa umepangwa kufanyika katika kambi ya jeshi la anga la Marekani ya Vandenberg mjini California.

Soma pia:Korea Kusini yasitisha mkataba wa kijeshi na Korea Kaskazini

Wizara ya ulinzi ya Korea Kusini imesema katika taarifa yake kuwa, urushaji wa satelaiti ulichelewa kutokana na hali mbaya ya hewa. Maafisa wa wizara wameongeza kuwa, urushaji huo umepangwa kufanyika tena Jumamosi ijayo.