1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Pyongyang yadai kunasa picha za satelaiti yake ya kijasusi

25 Novemba 2023

Vyombo vya habari vya serikali ya Korea Kaskazini vimetangaza leo kuwa kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un, amepitia picha zilizopigwa na satelaiti mpya ya kijasusi.

https://p.dw.com/p/4ZRE6
Nordkorea | Nordkoreanischer Führer Kim Jong-un
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akizungumza na maafisa wa kijeshi wakati akiangalia picha hizo zilizonaswa na Satelaiti ya kijasusi: 25.11.2023Picha: YONHAPNEWS AGENCY/picture alliance

Satelaiti hiyo imegundua sehemu mbalimbali za kimkakati kama kambi za jeshi la Marekani na maeneo kadhaa huko Korea Kusini. Lakini Seoul imesema ni mapema mno kubaini ikiwa satelaiti hiyo inafanya kazi kama anavyodai jirani yake Pyongyang.

Hata hivyo, wanadiplomasia wakuu wa Marekani, Korea Kusini na Japan wamefanya mazungumzo ya simu kulijadili tukio hilo ambalo pia wameliGuterres alaani hatua ya Korea Kaskazini ya kurusha satelaiti ya kijasusi katika mzingo wa dunialaani vikali.

Soma pia:Guterres alaani hatua ya Korea Kaskazini ya kurusha satelaiti ya kijasusi katika mzingo wa dunia 

Wataalamu wanasema kitendo cha Korea Kaskazini kurusha satelaiti ya upelelezi inayofanya kazi, kutaboresha uwezo wa taifa hilo wa kukusanya taarifa za kijasusi hasa kumhusu jirani yake Korea Kusini, na kutoa taarifa muhimu katika mzozo wowote wa kijeshi.