1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiongozi wa kijeshi Niger ziarani Mali na Burkina Faso

24 Novemba 2023

Kiongozi wa kijeshi wa Niger Jenerali Abdourahmane Tiani amekutana jana jioni na viongozi wenzake wa Burkina Faso na Mali katika ziara yake ya kwanza kimataifa tangu kutwaa mamlaka mwezi Julai mwaka huu.

https://p.dw.com/p/4ZOhR
Kiongozi wa kijeshi wa Niger Jenerali Abdourahmane Tiani akiwa na maafisa wengine wa kijeshi
Kiongozi wa kijeshi wa Niger Jenerali Abdourahmane Tiani akiwa na maafisa wengine wa kijeshiPicha: Balima Boureima/REUTERS

Mjini Bamako, Tiani amemshukuru mwenzake wa Mali Kanali Assimi Goita kwa msaada na uthabiti wa mamlaka na watu wa Mali kwa kushirikiana  na watu na mamlaka ya Niger bila kujali vikwazo.

Mwezi Septemba, Niger, Mali na Burkina Faso zilitia saini makubaliano ya pamoja ya ulinzi.

Soma pia:Jeshi la Mali liliukamata mji wa kimkakati wa Kidal ambao ulikuwa ngome ya waasi wa Tuareg na kudai kukuta kaburi la pamoja

Ikulu ya Ouagadougou imefahamisha kuwa Tiani pia amekutana kwa mazungumzo nakiongozi wa Burkina FasoKapteni Ibrahim Traore na wamejadiliana kuhusu mahusiano kati ya mataifa hayo mawili, masuala ya kijamii na kiuchumi pamoja na yale kupambana na ugaidi.

Kwanini Umoja wa Mataifa unashindwa kumaliza mizozo duniani?