1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mali yadai kuikomboa Kidal kutoka kwa waasi wa Tuareg

14 Novemba 2023

Jeshi la Mali limetangaza kuwa limechukua udhibiti wa mji wa kaskazini wa Kidal hiyo ikiwa ni mara ya kwanza kwa vikosi vya nchi hiyo kuikamata ngome muhimu ya waasi wa Tuareg katika kipindi cha karibu muongo mzima.

https://p.dw.com/p/4Yo3A
Mali Kidal | Rebellengruppe CMA
Picha: SOULEYMANE AG ANARA/AFP/Getty Images

Taarifa za kukombolewa kwa mji huo zimetolewa na kiongozi wa mpito wa Mali Kanali Assimi Goita kupitia mitandao ya kijamii na ujumbe rasmi wa ofisi yake uliosomwa moja kwa moja kwenye  televisheni ya taifa.

Soma pia: Jeshi la Mali lapambana na waasi karibu na mji wa Kidal

Kwa mujibu wa kiongozi huyo mafanikio hayo yamepatikana baada ya jeshi kufanya operesheni nzito iliyoyasambaratisha makundi ya wapiganaji wa Tuareg.

Kwa siku kadhaa sasa jeshi la Mali likisaidiwa na mamluki wa kundi la Wagner limekuwa likipambana na waasi wa Tuareg kuwania mji huo baada ya kuondoka kwa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa.