1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfghanistan

Kiongozi wa juu Afghanistan ataka uhusiano mzuri kimataifa

6 Aprili 2024

Kiongozi wa juu nchini Afghanistan amewarai raia nchini humo kuheshimu sheria ya kiislamu na kutoa wito wa mahusiano mazuri na jumuiya ya kimataifa, katika ujumbe wa nadra wa kuadhimisha kumalizika kwa mwezi wa Ramadhan.

https://p.dw.com/p/4eV8x
Afghanistan inavyoonekana majira ya baridi ya 2024
Raia nchini Afghanistan wametakiwa kuheshimu sharia ili kuepusha machafuko, kama mwanamke huyu aliyevalia Burqa ambalo ni vazi linalikubalika.Picha: Omer Abrar/AFP/Getty Images

Kiongozi huyo wa juu kabisa nchini Afghanistan, Hibatullah Akundzada amesema kwenye ujumbe wa maandishi kabla ya sikukuu ya Eid el Fitr wiki ijayo kwamba udhalimu na kuipuuza Sharia huvuruga usalama.

Hibatullah, anayeishi Kandahar na ambaye huonekana kwa nadra hadharani amerudia kusema mamlaka za Taliban zinataka uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi na mataifa mengine. 

Mwezi Januari kulisambaa ujumbe wa sauti uliohusishwa na kiongozi huyo, akiaapa kutumia adhabu zilizotumiwa na utawala uliopita wa Taliban kama ya kuwapiga mawe wanawake wazinifu, matamshi yaliyokosolewa vikali na makundi ya haki za binaadamu na Umoja wa Mataifa.