KINSHASA: Makundi matatu ya waasi yaweka silaha zao chini
27 Julai 2006Matangazo
Makundi matatu ya waasi katika eneo la mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo yamekubali kuweka silaha zao chini na kuwaruhusu wapiga kura kushiriki katika uchaguzi utakaofanyika Jumapili ijayo nchini humo.
Msemaji wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Kongo, Kemal Saiki, amesema mamia ya waasi hao watajumuishwa katika jeshi la taifa kwa kuruhusu uchaguzi ufanyike mkoani Ituri.
Waangalizi wa uchaguzi wa Kongo kutoka Umoja wa Ulaya bado wanaonya kuhusu matatizo ya maandalizi kabla uchaguzi kufanyika.